MOFULIMultibusiness & Services

Chagua rangi za tovuti. Chaguo lako linakumbukwa kwenye kifaa hiki.

EN

Kituo cha msaada

Tukusaidie nini?

Majibu kuhusu MOFULI, AFMIND, MOFPORT na MOFULI TV, pamoja na ushauri wa biashara wa vitendo. Msaada huu huu unapatikana kupitia kitufe cha ✦ kwenye kila ukurasa.

MOFULI ni nini?
MOFULI Multibusiness & Services ni kampuni ya Dar es Salaam inayofanya kazi katika huduma za biashara, ukuzaji wa michezo, teknolojia na habari. Inaendesha AFMIND, MOFPORT na MOFULI TV. Usajili: BRELA 630591, Baraza la Michezo la Taifa NSC 15069.
Ninajisajilije AFMIND (drafti)?
Usajili unafanyika kwenye jukwaa la AFMIND: afmind-league.web.app/sajili. Unajumuisha utambulisho, malipo na kitambulisho chako cha mchezaji. Soma mkataba wa mchezaji kwanza.
Nitajifunza wapi kanuni za drafti?
Ukurasa wetu wa drafti unaeleza historia, kanuni, aina na mbinu, na una ubao wa mazoezi unaoweza kucheza kwenye kivinjari.
MOFPORT ni nini na ninaanzaje?
MOFPORT ni mfumo wa MOFULI wa kusimamia bodaboda, bajaji, Noah, magari na malori. Sajili kampuni yako mofuli.co.tz/mofport, thibitisha barua pepe, na MOFULI ikihakiki nyaraka zako utapokea ufunguo wa majaribio wa siku 7 kwa barua pepe na SMS.
Mfumo wangu wa MOFPORT umejifunga. Nifanye nini?
Muda wa leseni umeisha. Kwenye app ya kampuni fungua Leseni, lipia kifurushi kwa MOFULI 0610 154 907, weka namba ya muamala, na utapokea ufunguo mpya wa mara moja (MFP-…) kwa barua pepe na SMS. Taarifa zako ziko salama wakati mfumo umejifunga.
Dereva anaweka vipi app ya MOFPORT?
Kampuni ikimaliza kusajili dereva, dashibodi inaonyesha QR, kitufe cha kupakua APK na msimbo wa herufi 8. Dereva anaweka MOFPORT Dereva, anaandika msimbo, anaingia kwa nywila ya ofisi na kuruhusu Location.
Je, kufuatilia dereva ni halali na kwa faragha?
MOFPORT inakusanya mahali tu kati ya “Anza zamu” na “Maliza zamu”, baada ya ridhaa ya dereva, kukiwa na alama inayoonekana. Pointi za GPS zinahifadhiwa miezi sita, kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania (2022).
Ninabadilishaje rangi za tovuti hii?
Gusa kitufe cha ◐ juu. Chagua Usiku, Bahari, Machweo, Dhahabu, Neon au Mchana. Chaguo lako linakumbukwa kwenye kifaa hiki.
MOFULI TV iko wapi?
Video ziko mofuli-live.web.app. Moja kwa moja inaonekana tu kipindi kikiwa hewani.
Je, MOFULI inaweza kuandaa mashindano au tukio letu?
Ndiyo. Dawati la matukio linapanga siku za mashindano, maafisa, usajili, tiketi na habari. Tuma tarehe, mahali na idadi inayotarajiwa ya washiriki kupitia ukurasa wa mawasiliano.