MOFPORT

SERA YA FARAGHA · TOLEO LA 20 OKTOBA 2026

Faragha yako kwenye MOFPORT

Sera hii inaeleza jinsi MOFPORT, mfumo wa kusimamia vyombo vya usafiri unaotolewa na MOFULI Multibusiness & Services (BRELA 630591, Dar es Salaam, Tanzania), unavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa binafsi. Tunazingatia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania, 2022, na kanuni zake.

1. Nani anafanya nini

2. Taarifa tunazokusanya

Kuhusu naniTaarifaKwa nini
Kampuni na mmilikiJina la kampuni au la mmiliki, TIN, BRELA, leseni ya biashara, NIDA na nakala za nyaraka, simu, barua pepe, anwani, nembo, IP na mahali pa ofisi (kwa ruhusa ya kivinjari)Kuhakiki kuwa kampuni ni halali, kufungua akaunti, mawasiliano, usalama
MaderevaJina, simu, barua pepe (hiari), NIDA, leseni ya udereva na picha yake, hesabu za kila siku, deni, alama ya utendajiKumtambua dereva, hesabu na usimamizi wa kazi kwa niaba ya kampuni
Mahali (GPS)Mahali, kasi na umbali wa chombo kati ya "Anza zamu" na "Maliza zamu" tu, pamoja na mahali pa simu inapounganishwa mara ya kwanzaUsalama wa chombo na dereva, hesabu za km, tahadhari za kasi, SOS
VyomboNamba za usajili, bima, LATRA, ukaguzi, picha za chombo, odometer, risiti za mafuta, picha za vipuri, service na matumiziVikumbusho vya nyaraka, faida ya chombo, kuzuia udanganyifu
MalipoKifurushi, kiasi, njia na namba ya muamalaKutoa ufunguo wa leseni na risiti

3. Ufuatiliaji wa madereva

4. Uchambuzi wa picha kwa AI

Kipengele hiki kikiwa kimewashwa (mmiliki wa kampuni anaweza kukizima wakati wowote kwenye kichupo cha "AI ya picha"), picha za odometer, vipuri na risiti za mafuta hupelekwa kwa mtoa huduma wa AI (Google Gemini, au Anthropic Claude) ili kusoma namba, kutambua kipuri au kusoma risiti. Picha nyingine (za chombo, nyaraka, matatizo) hazipelekwi. Matokeo yanasaidia ofisi kuhakiki, na uamuzi wa mwisho unafanywa na mtu. Tunapotumia kiwango cha bure cha Google Gemini, masharti ya Google yanairuhusu kutumia maudhui yanayotumwa kuboresha huduma zake; picha hizi ni za vyombo, odometer, risiti na vipuri tu, na hatutumi majina wala namba za simu za madereva pamoja nazo.

5. Tunawapa nani taarifa

6. Muda wa kuhifadhi

7. Usalama

8. Haki zako

Una haki ya kujua taarifa zako tulizonazo, kuzipata, kuzirekebisha, kupinga matumizi fulani, kuomba zifutwe pale sheria inaporuhusu, na kulalamika kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC). Dereva anapaswa kuanza kwa kuwasiliana na kampuni yake; sisi tutasaidia kampuni kutekeleza ombi lake.

9. Mawasiliano

MOFULI Multibusiness & Services, Dar es Salaam · info@mofuli.co · 0610 154 907 · 0744 100 918.

10. Mabadiliko

Tukibadilisha sera hii, tutaweka toleo jipya hapa na kuwajulisha wamiliki wa kampuni kwa barua pepe au ndani ya app, kabla ya mabadiliko makubwa kuanza kutumika.